Picha za Matukio

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa ya Manyara, Simiyu na Mara

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage akizungumza na maafisa uandikishaji ngazi ya Kata, Bariadi Mji Mkoani Simiyu.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Mbarouk Salim Mbarouk amekutana na kuzungumza na wawakilishi wa wazee wa kimila Mkoani Manyara, akiwa na Mjumbe wa Tume, Jaji (Mst) Marystella Longway na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile. Mazungumzo hayo yalilenga kuwashirikisha wazee hao katika kufanikisha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani humo.

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Mst) Marystella Longway (hayupo pichani) ametembelea mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ngazi ya Waandishi Wasaidizi na BVR Kit Operators Mbulu TC na Mbulu DC.

Mjumbe wa Tume ya Taifa Uchaguzi, Mhe. Asina Omary akiwa na maafisa wa Tume kupitia Sachita 88.1FM, Mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kuhusu Uboreshaji wa Daftari kwenye Mikoa ya Manyara, Simiyu na Mara.

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Mhe. Balozi Ramadhani Omari Mapuri amewasili mkoani Mara na maafisa wa Tume ambako amemtembelea ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima na baadae akafungua semina ya wadau wa Tume kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Athumani Kihamia ametembelea na kukagua maandalizi ya Tume kushiriki maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nanenane eneo la Nyakabindi Wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Kituo cha NBC Mtaa wa Butiama, Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu.

Wananchi wakiendelea na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura cha Shule ya Msingi Kabarim Kata ya Kabarim Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *