Habari

Makamu Mwenyekiti wa Tume atembelea Kata ya Mlowa Bwawani kukagua maandalizi Uchaguzi Mdogo

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtera mkoani Dodoma anayewakilishwa na Afisa Uchaguzi wa Jimbo hilo Elizabenth Gumbo (kushoto) kabla ya kutembelea kata ya Mlowa Bwawani inayofanya Uchaguzi mdogo Agosti 12, 2018.

Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera, Elizabenth Gumbo (kushoto) akieleza maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kata ya Mlowa Bwawani kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (katikati).Kulia ni Mwanasheria wa NEC Hamidu Mwanga.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akimueleza jambo  Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo (kushoto) wakati alipotembelea kata ya Mlowa Bwawani. Kulia ni Mwanasheria wa NEC, Hamidu Mwanga.

Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hamidu Mwanga (katikati) akizungumza jambo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo nje ya jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino mkaoni Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk.

Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera, Elizabenth Gumbo (kushoto) akimueleza jambo  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ( wa pili kulia) kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kata ya Mlowa Bwawani kwenye ofisi ya Msimamizi  Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mlowa Bwawani (Cleopa Leuna ( wa tatu kulia na Luis Pearson).Kulia ni Mwanasheria wa NEC Hamidu Mwanga.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (wa pili kushoto) akimsaidia Msimamizi Msaidiz wa Uchaguzi Kata ya Mlowa Bwawani Luis Pearson, kuweka bango la Kituo cha kupigia kura  cha Shule ya Msingi Mlowa Bwawani.Kulia kwao ni  Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera Elizabenth Gumbo na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata hiyo  Cleopa Leuna.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) akishuhudia uwekaji wa mabango ya uchaguzi karibu na  Kituo cha kupigia kura  cha Shule ya Msingi Nyamalela ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani wa Kata ya Mlowa Bwawani.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (wa pili kulia) akiagana na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mlowa Bwawani baada ya kutembelea kata hiyo kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, 2018
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (wa pili kulia) akiagana na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mlowa Bwawani baada ya kutembelea kata hiyo kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, 2018.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk ametembelea kata ya Mlowa Bwawani katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera Elizabenth Gumbo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtera, Jaji Mbarouk ameridhishwa na maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo.

Jaji Mbarouk amewasisitiza wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo kutumia vipaza sauti kufikisha ujumbe kwa wananchi kwani njia hiyo itarahisisha kufikisha ujumbe wa uchaguzi kwa wananchi wengi zaidi wakiwemo wasiojua kusoma na kuandika badala ya kutegemea zaidi taarifa za mabango.

Akitoa taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo kwa niaba ya, Afisa Uchaguzi wa Jimbo hilo Elizabenth Gumbo alisema maandalizi ya Uchaguzi huo yanakwenda vizuri.

Alisema wameshapokea vifaa vya awali vya Uchaguzi ikiwemo mfano wa karatasi ya kupigia, mabango ya Uchaguzi, fomu za Uchaguzi, bahasha za karatasi za kura na fedha za bajeti ya Uchaguzi wa kata hiyo.

Gumbo alisema ameshavitaarifu vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya mawakala wa vyama vyao na kwamba wamewaomba wawsilishe na picha za mawakala hao na ratiba ya kuwaapisha inasubiri muda ambao watakapowasilisha orodha hiyo.

Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni kuhusu mabadiliko ya ratiba ya kampeni za vyama vya CCM na Chadema ambavyo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi wa kata hiyo kwa kuwa chama kimoja kimekataa kubadilisha ratiba yake ambayo tayari ilishakubaliwa na vyama vyote.

Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mlowa Bwawani Cleopa Leuna alisema kata hiyo ina vituo 19 vya kupigia kura na kuna vitu 12 12 viko kwenye maeneo ya wazi na vinahitaji kujengewa.

Kuhusu kamati za maadili, Gumbo alisema tayari imeshaundwa ingawa bado haijafanya kazi yoyote kwa kuwa hakuna malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa utaratibu ambayo yanahitaji kujadiliwa na kamati hiyo.

“Hadi sasa hatujapokea malalamiko yoyote isipokuwa wakati wa uteuzi wa wagombea kulijitokeza malalamiko walituandikia barua, tukawajibu kuwa hamtakiwi kutoa pingamizi kwa njia ya barua tukawataka wajaze Fomu Na. 9 ya malalamiko wakakataa, zaidi ya hayo hatukupata malalamiko yoyote” alisema Gumbo.

“Hakuna uvunjifu wa amani uliojitokeza kwenye kampeni hadi kufikia leo na kampeni zinakwenda vizuri hakuna Mahali ambako tumepata taarifa za vurugu ya aina yoyote, watu wanajitokeza kwenye kampeni ingawa kwenye kampeni za chama kimoja wanakuwa wengi ikilinganisha na chama kingine” alisema.

Jaji Mbarouk baada ya kupokea taarifa hizo alishuhudia uwekaji mabango ya uchaguzi, orodha ya wapiga kura na tangazao la uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura vya Shule ya Msingi Mlowa Bwawani na Kituo cha Shule ya Msingi Nyamalela.

Kata ya Mlowa Bwawani inashiriki katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu ambapo vyama vya CCM na Chadema ndivyo vilivyosimamisha wagombea kwenye uchaguzi wa diwani wa kata hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *