Taarifa kwa Umma

Maamuzi ya Tume kuhusu Rufaa ya Uchaguzi Mdogo wa Tarehe 19 Januari, 2019 Kata ya Magomeni

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Magomeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Tume imepokea rufaa hiyo kwa kuzingatia kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na kanuni ya 28(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015,
Rufaa hiyo iliwasilishwa na mgombea Udiwani wa Chama cha Wananchi (CUF) Ndg. Ngude Athumani Yusuph akitaka arejeshwe kuwa […]